NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL KAHAMA
Afisa mtendaji wa kata ya Mhongolo Boniphace Kisimbu pia ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Mhongolo amewasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kwani zoezi hilo linaendelea mpaka octoba 20, 2024 .
Akizungumza na Huheso Digital, octoba 12, 2024 katika kituo cha uandikishaji mhongolo afisa amesema wameweka mawakala wa vyama kusaidia katika mchakato wa uandikishaji.
Mwenyekiti wa serikali za mtaa, Emanuel Nangale, amesema kabla ya zoezi, walifanya mikutano zaidi ya sita ili kuhamasisha uandikishaji pia alisisitiza kwamba walemavu wote wanapata fursa ya kujiandikisha, na mmoja mwenye baiskeli ya walemavu atahakikisha anajiandikisha.
Nangale amewataka wananchi kujitokeza katika siku za mwanzo na kuacha tabia ya kusubiri siku za mwisho ili kuepuka kuachwa na zoezi hilo kwani hii ni fursa muhimu kwa wananchi na haki yao kupiga kura hivyo juhudi za kuhamasisha zinaendelea ili kuhakikisha kila mtu anashiriki katika mchakato huu.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kujiandikisha Kenga Marwa amesema alipata hamasa ya uandikishaji daftari la mpiga kura kupitia matangazo ya redio pia kupitia mikutano ya wananzengo ndio maana amekuja kujiandikisha.
Pia Christina Benard amekiri kupokea hamasa kutoka kwa viongozi wa mtaa huo na kusema wao wameamua kuja kujiandikisha ili kutimiza haki yao ya kikatiba
Zoezi hili la uandikishaji limeanza tarehe 11 octoba 2024 na litamalizika octoba 20, 2024 lengo ni kuwaandikisha wananchi wakazi wa maeneo husika ili wapate sifa za kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mtaa utakaofanyika novemba 27, 2024.
No comments:
Post a Comment