TANZIA: KHADIJA SHAIBU ( DIDA ) AFARIKI DUNIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 4 October 2024

TANZIA: KHADIJA SHAIBU ( DIDA ) AFARIKI DUNIA


Uongozi wa Wasafi Media Unasikitika Kutangaza Kifo Cha aliyekua Mtangazaji wa Kipindi Cha Mashamsham cha Wasafi FM Khadija Shaibu ( Maarufu kama Dida) .


Dida atakumbukwa kwa Uhodari wake na Ubora wake Kwenye Tasnia ya Habari, Uliompelekea Kuwa Mtangazaji Namba Moja wa Kike Nchini na Kuwa Kioo kwa Wanawake na Watangazaji Wengi waliokua wanamtazama kama Mfano .


Tunaungana na Ndugu , Jamaa na Marafiki Wote Kusheherekea Maisha Ya DIDA , Na Kuenzi Yale Mengi Mazuri aliyoyafanya Kwenye Jamii na Tasnia ya Uandishi wa Habari .


Tunamuombea Mungu ailaze Roho yake Mahala Pema Peponi , Amen . #KwaheriMalkiaWaKipaza #TutaonanaBaadae

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso