RAIS MWINYI: SMZ KUENDELEA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 1 October 2024

RAIS MWINYI: SMZ KUENDELEA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI


Rais wa Zanzibar Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali kuendelea na juhudi za kuleta Maendeleo wananchi katika kila sekta na kuwaomba kuunga mkono katika juhudi hizo.




Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 1 Oktoba 2024 wakati alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) , Tumbatu Jongowe Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Rais Dk Mwinyi amefahamisha kuwa lengo la Serikali ni kuona Wanafunzi nchi mzima wanasoma katika mazingira rafiki ,majengo ya kisasa yenye vifaa kamili vya kufundishia , maabara, vyumba vya Kompyuta .


Aidha Rais Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Serikali inakusudia kujenga hospitali ya Wilaya ili wananchi wa Tumbatu kuwa na Uhakika wa matibabu na kuwapunguzia gharama za kufuata matibabu katika maeneo mengine.


Akizungumzia suala la malezi ya vijana na Watoto ametoa wito kwa Wazazi kuweka mkazo katika kuwafundisha maadili na malezi bora ili wawe raia wema wa baadae .


Amesisitiza kuwa Amani ndio msingi wa Maendeleo ya nchi inayohitaji kuleta Maendeleo hivyo kila mmoja ana jukumu la kulinda Amani.


Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amewahakikishia wananchi wa Tumbatu kuwa Serikali itajenga skuli nyengine kubwa kisiwani humo ili kukidhi mahitaji na kuwawezesha Wanafunzi kusoma katika mazingira Bora.


Wakati huo huo Rais Dk. Mwinyi amekabidhi shillingi Milioni nane kwa Zawiyya nne za Tumbatu kwa ajili ya maandalizi ya Maulidi ya Mtume .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso