PPRA YATOA MAFUNZO YA UNUNUZI WA UMMA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 23 October 2024

PPRA YATOA MAFUNZO YA UNUNUZI WA UMMA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA SHINYANGA



Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati akifungua Mafunzo kuhusu Manunuzi ya Umma kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na PPRA




NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL SHINYANGA


Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari katika Mkoa wa Shinyanga ili kuboresha uelewa wa mifumo na taratibu za ununuzi wa umma.


Mafunzo haya yana lengo la kuwajengea waandishi uelewa wa kina kuhusu sheria na mifumo ya ununuzi, ikiwa ni pamoja na Mfumo wa NeST (National e-Procurement System of Tanzania).


Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo leo Oktoba 23,2024 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro amesisitiza umuhimu wa waandishi katika kusimamia uwajibikaji wa matumizi ya fedha za umma.


Wakili Mtatiro ameeleza kuwa waandishi wanapaswa kuwa daraja kati ya serikali na wananchi, na kuelewa masuala ya ununuzi ni muhimu kwa maendeleo ya jamii.


Alfred Manda Nicodemus kutoka PPRA amebainisha kuwa, uelewa wa kanuni za ununuzi ni muhimu ili waandishi waweze kutoa habari sahihi na za kuaminika.


Patrick Mabula, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, ameongeza kuwa mafunzo haya yanaimarisha uelewa wa waandishi na kusaidia katika wajibu wao wa kutoa taarifa sahihi.


Amesema mafunzo hayo yatatoa mabadiliko chanya katika uandishi wa habari na kuongeza uelewa wa masuala ya ununuzi wa umma miongoni mwa waandishi wa habari katika Mkoa wa Shinyanga.






Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Patrick Mabula akitoa taarifa kuhusu mafunzo hayo
Mwezeshaji kutoka PPRA, Alfred Manda Nicodemus akielezea kuhusu PPRA na mfumo wa NeST
Mwezeshaji kutoka PPRA, Alfred Manda Nicodemus akielezea kuhusu PPRA na mfumo wa NeST
Mwezeshaji kutoka PPRA, Alfred Manda Nicodemus akielezea kuhusu PPRA na mfumo wa NeST

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso