NSSF KAHAMA YATOA VYETI KWA WANACHAMA NA WAAJIRI WANAOLIPA MICHANGO IPASAVYO KILA MWEZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 11 October 2024

NSSF KAHAMA YATOA VYETI KWA WANACHAMA NA WAAJIRI WANAOLIPA MICHANGO IPASAVYO KILA MWEZI

Meneja wa NSSF Mkoa wa Kahama Aisha Nyemba katikati akiwa na waajiri pamoja na wanachama katika picha ya pamoja

NA NEEMA NKUMBI-HUHESO DIGITAL KAHAMA

NSSF Mkoa wa Kahama imetoa vyeti na pongezi (certificate of Appreciation) kwa baadhi ya wanachama wa sekta binafsi wanaojilipia wenyewe kila mwezi bila kukosa.

Pongezi hizo zimetolewa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Kahama Aisha Nyemba octoba 11, 2024 katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika ofisini hapo.

Wanachama hao ni Benjamini Hosea, Costantina Ndazi, Donatira Feliciana, Emanuel Masembo na Esron Yuba

Pia wamewatunuku vyeti vya pongezi (certificate of Appreciation) waajiri mbalimbali kwa kutekeleza majukumu yao ya kulipa michango ya wanachama kwenye mifuko kwa wakati.

Miongoni mwa waajiri hao ni Bulyanhulu Gold Mine ambayo inachangia shilingi bilion 1.5 na inawanachama 1380, MSA Laboratories (T) LTD ambayo inachangia shilingi milion 50 na inawanachama 102, Msalala Gold Limited na SHIDEPHA+KAHAMA.

Wengine ni ST Josephine Bakhita English Medium P/school, Freemanga Company Limited, ST Clement English Medium Pre and Primary school Rocken Hill Academy, Prostero Investiment and General Traders LTD.

Pia SASAGI OIL, Pangea Mineral Limited, SAINT Bernard Medical Dispensary Frester Investment CO.LTD, na ST ann's Dispensary.

Aidha Aisha amewataka wanachama kuwa mabalozi kwa wengine ilikufikia adhma ya serikali ya 'Hifadhi ya jamii kwa wote'.

Hata hivyo Aisha  amesema mfuko wa Nssf umewekeza katika kuboresha mifumo ya TEHAMA ili kuwafikia wanachama kwa urahisi.

Wiki ya huduma kwa wateja ilianzishwa rasmi kimataifa mwaka 1987 kwa lengo la kutambua umuhimu wa huduma bora kwa wateja na juhudi za wafanyakazi wanaotoa huduma bora kwa wateja.

Maadhimisho ya huduma kwa wateja yalianza tarehe 7 oktoba 2024 yenye Kauli mbiu 'Huduma Bora Popote ulipo'
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kahama Aisha Nyemba katikati akiwa na waajiri pamoja na wanachama katika picha ya pamoja
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kahama Aisha Nyemba katikati akiwa na waajiri pamoja na wanachama katika picha ya pamoja
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kahama Aisha Nyemba katikati akiwa na waajiri pamoja na wanachama katika picha ya pamoja
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kahama Aisha Nyemba akikabidhi vyeti kwa wanachama 

Meneja wa NSSF Mkoa wa Kahama Aisha Nyemba akikabidhi vyeti kwa wanachama 

Meneja wa NSSF Mkoa wa Kahama Aisha Nyemba akikabidhi vyeti kwa wanachama 
Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja katika ofisi za NSSF Kahama
Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja katika ofisi za NSSF Kahama

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso