MIFUMO IMARA YA GRIDI INAIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME - DKT. BITEKO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 24 October 2024

MIFUMO IMARA YA GRIDI INAIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME - DKT. BITEKO




📌 *Asema Gridi zenye ufanisi ni injini ya uchumi wa nchi*


📌 *Tanzania yaendelea kuwekeza kwenye teknolojia za Gridi imara*



Singapore



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema uwepo Gridi imara kwenye nchi unasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuinua sekta ya nishati na uchumi wa Taifa kwa ujumla.


Ameeleza hayo wakati akizungumza kwenye Jukwaa la Wadhibiti wa Huduma za Nishati kwa Ukanda wa Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) wakati wa Mkutano wa Wiki ya Nishati nchini Singapore.


Amesema kuwa, Serikali ya Tanzania inawekeza kwenye teknolojia za gridi imara kupitia miradi ya kuimarisha gridi na kuwa na ushirikiano wa kikanda na nchi jirani kama Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Zambia, Msumbiji na Uganda.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Joseph John Kilangi amesema Tanzania imeweka jitihada kubwa kuboresha mfumo wake wa gridi ya Taifa kwa kuweka miundombinu ya kutosha.


‘’Nipende kuwajulisha kuwa Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya kuimarisha gridi ikiwemo kubadilisha miundombinu chakavu na kubuni Teknolojia ( Smart Technology) ili kuchambua mifumo ya data na kupunguza upotevu wa umeme.’’ Amesema Kilangi.


Kuhusu Nishati Safi, Kilangi amesema Tanzania kama ilivyo nchi nyingi zinazoendea, inasisitiza matumizi ya nishati mbadala kama chanzo muhimu cha umeme na kusisitiza umuhimu wa mifumo ya udhibiti inayovutia uwekezaji na ushirikiano wa kimataifa katika kushughulikia changamoto za nishati.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso