MHE NDEJEMBI - HALMASHAURI, TUMIENI MAPATO YA NDANI KUMALIZIA MAJENGO YALIYOANZISHWA KWA NGUVU ZA WANANCHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 8 October 2024

MHE NDEJEMBI - HALMASHAURI, TUMIENI MAPATO YA NDANI KUMALIZIA MAJENGO YALIYOANZISHWA KWA NGUVU ZA WANANCHI


Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa Deogratius Ndejembi akikagua vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Mapamba


NA NEEMA NKUMBI-HUHESO DIGITAL USHETU

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amezitaka Halmashauri kuunga mkono juhudi za Rais Samia kwa kutenga fedha za mapato ya ndani kumalizia madarasa ambayo yameanzishwa kwa nguvu za wananchi.

Agizo hilo amelitoa oktoba 7, 2024 alipotembelea mradi wa maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne katika shule ya Sekondari Mapamba iliyopo Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama.

"Hela ambazo mlikuwa mnaweza kutenga kabla serikali haijaleta fedha, mlikuwa mnaweza kutekeleza majukumu yenu lakini baada ya Rais kuleta pesa za serikali mmeacha majukumu yenu kwa hiyo malizieni madarasa wananchi waone jitihada za serikali", amesema Mhe. Ndejembi.


Mkuu wa Mkoa Anamringi Macha amepongeza juhudi za Rais Samia kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo hata vijijini sasa kuna madarasa ya kisasa yenye feni na mazingira waliokuwa wanayaona mjini hata kijijini sasa yapo.


Naye Mbunge wa Ushetu Mhe Emanuel Peter Cherehan ameunga mkono juhudi za Rais Samia kwa kuchangia shilingi milion tano (5) kwa ajili wa umaliziajia wa ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Mapamba


Awali akisoma Taarifa ya ujenzi wa madarasa manne ya shule hiyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mapamba,Mwalimu Rahel Wilson amesema shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa jengo rasmi la utawala , Nyumba za Walimu pamoja na ukamilishaji wa Maabara ya Fizikia.

Mradi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mapamba unagharimu jumla ya Shilingi Milioni 116 na laki tano ambapo mpaka sasa zimetumika Shilingi Milioni 98.8 na kubakia ni milioni 17.6.

Muonekano wa vyumba vya madarasa vinavyoendelea kumaliziwa


Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa Deogratius Ndejembi akikagua vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Mapamba

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso