MHE. MCHENGERWA; ARUSHA DC ZINGATIENI VIGEZO VYA KUWA MJI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 3 October 2024

MHE. MCHENGERWA; ARUSHA DC ZINGATIENI VIGEZO VYA KUWA MJI



OR-TAMISEMI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaelekeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuzingatia vigezo vilivyowekwa kisheria ili kupata hadhi ya kuwa Mji na sio kuanzisha Mamlaka ya Mji mdogo kama walivyopendekeza.


Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake Kwenye Halmashauri hiyo kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri hiyo.


Amesema "Nimepokea ombi lenu la kutaka kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo na hatimaye kuwa na Manispaa huko mbeleni lakini ninachoweza kuwashauri kwa sasa ni kuwa zingatieni vigezo na sifa za Halmashauri ya Mji na mkijitathimini kama mmekidhi wasilisheni mapendekezo hayo Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa ajili ya hatua zaidi!


“Kuwa na mamlaka ya mji mdogo sio kitu ninachopendekeza sana kwa sababu kwanza inahitaji kulelewa na Halmashauri ya Wilaya hivyo katika mapato yenu mtatoa fedha kwa ajili ya kuendesha mamlaka ya mji mdogo na kwenda kuwa Manispaa mtakua mmevuka hatua ya kuwa Mamlaka ya Mji kama mnadhani mna sifa hizo wasilisheni maombi yenu yakiwa yamepita kwenye vikao vyote muhimu na yakifika Ofisi ya Rais - TAMISEMI tutayachambua kama mmekidhi vigezo mtapa hadhi ya Mji,"amesema.


Aidha ameongeza kuwa changamoto zilizowasilishwa amezipokea hususan ikiwamo ya miundombinu ya barabara za lami na kuahidi kufanyia kazi.


Waziri Mchengerwa yupo kwenye ziara ya Kikazi mkoani Arusha na atatembelea Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Meru pamoja na Jiji la Arusha.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso