Mdau wa Maendeleo Mbogwe Aibeba Shule ya Msingi Nyakafulu kwa Mchango wa Shilingi 700,000
Na Paul Kayanda, Geita
PIUS Zacharia Lukaga ameonyesha moyo wa kujitoa kwa maendeleo ya elimu baada ya kuchangia shilingi 700,000 katika mahafali ya Shule ya Msingi Nyakafulu iliyopo Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita ambapo alialikwa kama mgeni rasmi.
Mchango huo mkubwa ulitolewa kufuatia risala ya wanafunzi iliyobainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo, ikiwa ni pamoja na upungufu wa huduma ya chakula na mashine ya photocopy iliyoharibika.
Kufuatia hafla hiyo, Lukaga aliwaomba wazazi na wageni waliohudhuria kuchangia, ambapo walifanikiwa kukusanya shilingi 200,000. Lukaga aliongeza shilingi 500,000 kutoka mfukoni mwake, na kufanya kuwa mla ya shilingi 700,000.
Mchango wake umepokelewa kwa shangwe na jamii ya Nyakafulu, ikiwa ni ishara ya matumaini mapya kwa kuboresha duala la elimu.
Aidha Lukaga pia alihimiza ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuhakikisha maendeleo endelevu.
Hata hivyo Lukaga aliwashukuru waliojitolea na akasisitiza kuwa ushirikiano ndiyo njia pekee ya kuleta mafanikio ya kudumu kwenye sekta ya elimu katika Wilaya ya Mbogwe na Mkoa wa Geita kwa ujumla
No comments:
Post a Comment