MASUDI KIBETU AFUNGUA MAFUNZO YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WILAYA YA KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 25 October 2024

MASUDI KIBETU AFUNGUA MAFUNZO YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WILAYA YA KAHAMA




Na. Paul Kasembo, KAHAMA.

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ndg. Masudi Kibetu amefungua mafunzo ya viongozi wa Vyama vya Siasa Wilaya ya Kahama na kuwaomba kuendeleza amani, upendo na mshikamano kama ilivyo sasa hivi kwani wanapaswa kuendelea na maisha baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopo mbele yao.


Kibetu ameyasema haya leo tarehe 24 Oktoba, 2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambapo jumla ya Vyama 16 vya Siasa vimehudhuria Mafunzo ili kufahamu Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.


"Niendelee kuwaomba na kuwasisitiza tena kuwa, kama ambavyo tunavyoishi hivi sasa kwa upendo, umoja na mshikamano wetu tuendelee nao wakati na baada ya uchaguzi kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi huu," amesema Kibetu.




Awali akitoa Elimu hii kwa wajumbe, Frank Shija ambaye ni mwezeshaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kuwa, viongozi wanapaswa kuzisoma na kuzielewa vema Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Ofisi ya Msajili ili ziweze kuwasaidia na kuwaepusha kutenda makosa ambayo yanaweza kuepukika na kwamba uzalendo, utu na hekima vikawe sehemu ya kampeni zao hata baada ya uchaguzi.


Kwa upande wao viongozi wa vyama vya siasa kwa nyakati tofauti wameiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhakikisha kunakuwa na usawa kabla, wakati na baada ya uchaguzi huu kwani ofisi hiyo ndiyo mlezi wa vyama vyote huku wakisisitiza kuwa wanayo imani kubwa na Msajili wa Vyama huku wakiiomba iwe na utaratibu wa kushuka ngazi za chini kukutana na kuzungumza na viongozi hawa kama walivyofanya hivi sasa au kusubiria mpaka kutokee uchaguzi kama hivi.


Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania inaendelea na zoezi la utoaji wa elimu na mafunzo kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhusu Sheria zinazosimamiwa ambapo walengwa ni viongozi wa vyama hivi vya siasa ikiwa ni kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka huu.



@orpptanzania

@kahamamc_official

#shinyanga_rs

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso