MAJALIWA MGENI RASMI SIKU YA MWALIMU DUNIANI BUKOMBE 2024. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 11 October 2024

MAJALIWA MGENI RASMI SIKU YA MWALIMU DUNIANI BUKOMBE 2024.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Octoba 11, 2024 amewasili mji mdogo wa Ushirombo, Wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo atakuwa Mgeni Rasmi katika Siku ya Mwalimu Duniani kwa mwaka 2024.


Maadhimisho hayo yanafanyika kwenye Viwanja vya shule ya Sekondari Ushirombo ambapo pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Waziri Mkuu atakabidhi vifaa vya kujifunza na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi wilayani humo.


Mheshimiwa Majaliwa amepokelewa na Mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe, ambaye ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso