Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila amemtaka RAS Dodoma na Pwani kuyatunza magari waliyokabidhiwa ili yadumu na kutumika katika kuimarisha usafi wa mazingira na maji kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Mhandisi Mativila ametoa maelekezo hayo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, wakati akikabidhi magari 2 kwa mikoa ya Dodoma na Pwani yaliyotolewa na Serikali ili kusimamia na kuimarisha usafi wa mazingira na maji katika mikoa hiyo.
“Ninawaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa ya Dodoma na Pwani niliowakabidhi magari haya kuhakikisha wanasimia yafanye kazi ya kuboresha huduma za afya na usafi wa mazingira,” Mha. Mativila amesisitiza.
Sanjari na hilo, Mha. Mativila amesisitiza magari hayo yasiende kutumiwa katika shughuli ambazo hazijakusudiwa na Serikali, hivyo yakatumike kuimarisha usimamizi wa usafi wa mazingira na maji katika mikoa ya Dodoma na Pwani.
6
Aidha, Mha. Mativila amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji na vyoo bora katika shule 362 na katika vituo 338 vya kutolea huduma za afya ndani ya mwezi mmoja kwani fedha zimekwishatolewa na Serikali.
No comments:
Post a Comment