DIDA KUZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 5 October 2024

DIDA KUZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU



Mtangazaji wa Kipindi cha Mashamsham cha WasafiFM Khadija Shaibu maarufu kama Didah, ambaye amefariki dunia jioni ya jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa, anatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es salaam.


Mtangazaji mwenzake wa kipindi cha Mashamsham, Idris Kitaa amesema “Dada aliumwa hapa katikati lakini haikuwa kwa muda mrefu ilikuwa kwa muda mfupi ndani ya wiki , wiki mbili hivi na kitu kikubwa kilichokuwa kinamsumbua ni vidonda vya tumbo ambavyo nafikiri vimepelekea umauti wake, Mungu mwenyewe ndio anajua zaidi”


“Tutampumzisha kwenye makazi yake ya milele saa 10 Jioni katika makaburi ya kisutu sehemu ambayo amehifadhiwa pia Mama yake”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso