WATANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA VIFAA VYA UMEME VYENYE THAMANI TA SHILINGI MILIONI 54. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 12 September 2024

WATANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA VIFAA VYA UMEME VYENYE THAMANI TA SHILINGI MILIONI 54.


Watu watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kahama kwa kosa la kuhujumu uchumi kwa kuunda genge la uhalifu na wizi wa nyaya za umeme aina ya Alminiam zenye thamani ya Sh.milioni 54.


NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA

Wakisomewa mashtaka hayo septemba 12, 2024 na Mkuu wa Mashtaka Ofisi ya Kahama, Jukaeli Jairo aliiambia mahakama kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo Septemba tatu mwaka huu katika miji ya Kahama na Dar es Salaam ambapo walikutwa na gram tatu za nyaya ya Almininu.


Jairo amesema, watu hao wanakabiliwa na makosa mawili, kosa la kwanza ni kuunda genge la uharifu kwa makusudi kinyume na sheria 4(1)(a) inayosomwa pamoja na sheria namba 57(1) na 60(2) ya sheria ya uhujumu uchumi, huko kosa la pili likiwa ni wizi kinyume na kifungu cha sheria namba 258(1)(2)(a) na 265 ya kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.


Aidha amewataja watuhumiwa  hao kuwa ni pamoja na; Erick Kamuhanda Rweyemamu(36), Kaijage Kagenyi(27),Carlos Eck Chamanga(29), Ngwea Mkomwa Sufian(29),wote wakiwa ni mafundi umeme pamoja na  Lemi Paul Mtwale(34) Mkandarasi wa umeme.


Kesi hiyo  namba 26208/2024 ilisikilizwa na Hakimu Mkazi mwandamizi wa Wilaya ya Kahama Edmund Kente na mzigo iliyoibiwa ilikuwa mali ya Iddcon Investment Limited aliyekuwa akitekeleza mradi wa Rea katika kata ya Idahina Halmashauri ya Ushetu.


Watuhumiwa wote hawakutakiwa kujibu chochote katika kosa la kwanza na kosa la pili walikana mashtaka ambapo waliiomba Mahakama dhamana lakini dhamana  ilishindikana kwa kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo la Uhujumu uchumi na kesi itatajwa tena  septemba 27 mwaka huu.







No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso