Na WAF - Manyara
Wananchi wa Mkoa wa Mnyara wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa kambi ya siku sita ya matibabu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia kwa kufika katika hospitali zote za halmashauri ya zao ili kupatiwa huduma za matibabu ya kibingwa kwa wagonjwa na kuangalia afya zao kwa wasio na changamoto za kiafya.
Wito huo umetolewa Septemba 23, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mjini Mhe. Emmanuela Kaganda kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga wakati akiwapokea na kufungua Kambi ya Matibabu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia katika Hospitali ya Wilaya ya Babati Mjini, iliyowekwa katika Mkoa huo kuanzia kwa siku sita kuanzia tarehe 23 hadi 28 Septemba, 2024.
Mhe. Emmanuela amesema ni vyema kwa wananchi wa Mkoa huo kutenga muda wao na kwenda katika hospitali walipo madaktari bingwa hao na kupima afya zao kwani kujua afya yako mapema kutasaidai kupatiwa matibabu mapema na kuebukana na athari zinazoweza kuepukika kutokana na magonjwa.
“Afya ya mwanadamu ilivyo unaweza ukawa unatembea ukajiona mzina kumbe ni mgonjwa hivyo upimaji wa awali unaweza kuwa mgumu ila matibabu yakawa rahisi ili kukichelewa sana upimaji unaweza kuwa rahisi ila matibabu yakawa magumu, hivyo nichukua fursa hii kutoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa manyara hasa wilaya ya Babaji mjini kutumia fursa hii ya madaktari bingwa wa Rais Samia kupima na kujua afya zetu ili ukibaiika unachangamoto za kiafya basi upatiwe matibabu ma madaktari hao.” Amesema Mhe, Emmanuela
Ameongeza kuwa serikali inayoongwaza na Rais Samia Suluhu Hassani inadhamira ya dhati ya kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za kibingwa karibu na eneo analoishi .
“Ni maono makubwa na mazuri ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi baada ya kushusha fedha nyingi na kujenga hospitali kubwa na nzuri, vituo vya kutolea huduma za Afya na zahanati katika kila mkoa na kusambaza vifaa tiba vya kisasa Pamoja na dawa ameona ni vyema kuwasongezea na kuwafikishia huduma za matibabu ya kibingwa karibu walipo watanzania na kuwatua mzigo wa gharama za matibabu wananchi hasa wa hali ya chini wasizifuate huduma hizo mbali ya maeneo yao.” Amesema Mhe. Emmanuela
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya. Bi. Gertrude Naphtali ambae ni Afisa Mbobezi Afya ya Jamii kutoka Idara ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto amesema seti ya madaktari bingwa 45 wamesambazwa katika hospitali zote za halmashauri za Mkoa wa manyara kwa ajili ya kutoa matibabu ya kibingwa wa Watanzania na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ii kupatiwa huduma za kibingwa.
“Madaktari watakaotoa huduma katika kambi hii ya siku sita hapa Manyara ni Daktari bingwa wa magonwa ya wanawake na Ukunga, Daktari bingwa au bobezi wa watoto na watoto Wachanga, Daktari bingwa wa upasuaji au Mfumo wa mkojo, Daktari bingwa wa usingizi na ganzi, Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani, Daktari bingwa wa kinywa na Meno, Muuguzi Bingwa na Daktari wa mifupa.”
No comments:
Post a Comment