Wanafunzi wameaswa kutokuishi maisha ya kuigiza bali wajitambue na kuwa na nidhamu pindi wakiwa shule hata watakapo hitimu masomo yao.
NA NEEMA NKUMBI- HUHESO DIGITAL BLOG USHETU
Hayo yamesemwa septemba 27, 2024 na Mkuu wa shule ya sekondari ya Igunda Mwalimu Zacharia Ngusa katika mahafali ya saba ya kidato cha nne yaliyofanyika katika shule hiyo.
"Wanafunzi mnapaswa kujitambua dunia ya leo imekuwa na mambo mengi kama wazazi au walimu hatuwezi kuwasaidia msipojitambua wenyewe kuwa ninyi ni akina nani na mnataka kuwa nani, muwe na nidhamu binafsi pia mjitahidi kupambana na changamoto za dunia kwani maisha sio rahisi", amesema Mwalimu Ngusa.
Mwalimu Ngusa amesema wanafunzi hawasomi ili kuepuka kazi bali wanasoma ili kufanya kazi zaidi hivyo kufanya kazi kwa bidii ni uzalendo wa kweli.
Pia Mwenyekiti wa Bodi ya shule Bulege Bitta amewaomba wazazi kushirikiana na bodi ya shule katika malezi ya wanafunzi kuwa na maadili na kuwapa wanafunzi wa kike haki zao za msingi kwani wazazi wanaachana na watoto wa shule wakiwa na miaka mitano mpaka wanapohitimu wanakuwa mikononi mwa walimu lazima waweke ushurikiano wa kutosha kwa walimu kwani watoto ni hazina ya kesho.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi Saada Rashidi amewasihi wanafunzi hao kuwa watulivu wakati wakisubiri matokeo yao kwani bado wanatakiwa kupambana ili kuweza kuvuna matunda ya masomo yao na kufikia malengo.
Awali akisoma risala katika mahafali hiyo Getruda Isaya ameeleza changamoto zinazoikabili shule hiyo ni ukosefu wa umeme hali inayopelekea kushindwa kusoma kwa njia ya kisasa kama komputa, projecta na kuchaji vifaa vya umeme.
Getruda ameeleza kuwa shule yao ina ukosefu wa bwalo, vifaa vya michezo pamoja na nyumba za walimu hali inayopelekea kuishi mbali na eneo la shule ambapo inapunguza ufanisi.
Akijibu risala, Diwani wa kata ya Igunda Tabu Katoto ambaye alimuwakilisha Mgeni rasmi katika sherehe hiyo Mbunge wa Ushetu Mhe Peter cherehani, amesema watashirikiana kujenga bwalo na nyumba za walimu kama walivyoshilikiana kujenga vyumba vya madarasa.
Shule ya Igunda ilianzishwa mwaka 2015, ina jumla ya wanafunzi 357,wavulana 141 na wasichana216, waliohitimu kidato cha nne ni wanafunzi 55 wasichana 33 na wavulana 22.
Diwani wa kata ya Igunda Mheshimiwa Katoto akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne katika shule wa sekondari Igunda

Wahitimu wa kidato cha nne wakiwalisha keki wazazi wao
Mwanafunzi wa kidato cha nne Getruda akisoma risala kwa mgeni rasmi akielezea mafanikio na changamoto mbalimbali katika shule ya Igunda
Mkuu wa Shule ya Igunda akiwahusia wanafunzi wake kujitambua na kuwa na nidhamu binafsi pia waache maisha ya kuigiza bali waishi uhalisia
No comments:
Post a Comment