Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa elimu maalumu kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia , Dk . Magreth Matonya akizungumza mkoani Arusha.
………………..
Happy Lazaro, Arusha .
Wakuu wa mikoa na wilaya nchini wametakiwa kufanya utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalumu.katika maeneo yao ili waweze kujulikana na kuweza kupata haki zao za msingi kwenye maeneo yaliyoanishwa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 30 ya elimu jumuishi yaliyofanyika katika chuo cha ualimu elimu maalumu Patandi kilichopo mkoani Arusha .
Amesema kuwa,bado kuna wananchi wengi ambao wanaendelea kuficha watoto wenye mahitaji maalumu na hivyo kuwasababishia haki zao za msingi kama wengine wanavyopata haki.hizo katika.vituo.mbalimbali.vilivyoanishwa.
“Wakuu wa mikoa na wilaya naombeni sana mtumie wataalamu wenu kusaidia kupata taarifa ya watoto wote wenye mahitaji maalumu na kama kuna mtoto ambaye amefichwa ili serikali iweze kuchukua hatua na kuwapatia haki zao za msingi.”amesema .
“Naombeni sana mfanye ufuatiliaji wa karibu ili kusiwepo kwa mtoto yoyote yule mwenye changamoto mhakikishe mnashirikiana wadau ili kupata idadi kamili ya watoto wenye mahitaji ili waweze kuhudumiwa kwa karibu kama wengine wanavyohudumiwa.”amesema.
Aidha amesema walimu waliopo katika kada hiyo ya elimu jumuishi wamekuwa wakijitolea sana na wanafanya kazi ngumu sana ,hivyo ni lazima wafanye kazi katika mazingira yanayoridhisha ili waendelee kuwahudumia watoto hao kwa karibu na kuwatatulia changamoto zao kwa wakati.
“Katibu mkuu sitaki kusikia mwalimu.yoyote ana changamoto kama ni kipaumbele naomba wapewe walimu hawa wa elimu.jumuishi kwani wanafanya kazi kubwa sana kwani kazi wanayofanya ni ibada pekee.”amesema .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa elimu maalumu kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia , Dk . Magreth Matonya amesema kuwa,serikali imekuwa ikitangaza fursa kubwa sana kwa watoto wa elimu.maalumu ambapo mtoto yoyote mwenye changamoto anapata huduma zote za msingi anazohitaji kupata.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule ya patandi elimu maalumu wameshukuru serikali kwa namna ambavyo imewekeza kwao na kuweza kuwapatia elimu wakiwa tangu wadogo na kuweza kutimiza malengo yao kwani walikuwa wamesahaulika kwa muda mrefu sana .
No comments:
Post a Comment