WAJASIRIAMALI, TUMIENI FURSA VIZURI - RC MACHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 9 September 2024

WAJASIRIAMALI, TUMIENI FURSA VIZURI - RC MACHA




Na. Paul Kasembo, SHY RS.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamiringi Macha amewataka wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za ngozi katika Halmashauri ya Manispaa yq Shinyanga kutumia vizuri fursa za upatikanaji wa ngozi kutokana na machinjio ya wanyama yaliyopo Mkoa wa Shinyanga kutengeneza bidhaa nyingi zaidi na hivyo kukuza uchumi wa Taifa.




Ameyasema hayo leo tarehe 9 Septemba, 2024 wakati akifungua mafunzo ya wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za ngozi Manispaa ya Shinyanga ambayo yanaratibiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yanafanyika kwa siku (2) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wataalam mbalimbali kutoka TAMISEMI, SIDO, TBS, wadau nk huku akisisitiza ubunifu zaidi.




“Ningependa kuwaasa mjitahidi kutumia vizuri fursa za upatikanji wa ngozi kwa sababu ndani ya Mkoa wa Shinyanga kuna machinjio ya wanyama mbalimbali kama ng’ombe, mbuzi na kondoo ambayo kupitia machinjio haya mnaweza mkapata kiasi kikubwa cha ngozi na mkafanikiwa kutengeneza bidhaa nyingi zaidi na kupata faida kubwa hatimaye kukuza uchumi wetu na Serikali pia kongeza pato lake hapo,” amesema RC Macha.




Kwa upande wake meneja wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kitengo cha Tafiti na Mafunzo Mwl. Hamisi Mwanasala amesema mafunzo haya yamelenga kuwafikia wajasiriamali takribani 40 wanaojishughulisha na bidhaa za ngozi na amewataka washiriki wote kutumia vema mafunzo haya ili kuboresha bidhaa wanazozalisha ziendane na viwango vya TBS.




“Mafunzo haya yamekusudia kuwasaidia wajasiriamali wanaojishughulisha na bidhaa za ngozi takribani 40 ili waweze kuboresha bidhaa zao za ngozi ziendane na viwango ambavyo Shirika la Viwango Tanzania limethibitisha ili kukuza soko la ngozi nchini” amesema Hamisi.




Mafunzo haya ya wajasiriamali yatafanyika kwa siku mbili kuanzia leo Jumatatu tarehe 9 Septemba, 2024 hadi Alhamis tarehe 10 Septemba, 2024 mafunzo ambayo yanatajwa kuwa yenye tija zaidi kwani yatawaongezea ujuzi na maarifa na kwenda kuchechemua uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.



@tbs_viwango @julius_mtatiro @shinyangamanispaa #shinyanga_rs

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso