Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha vifo vya Wajawazito vinavyotokana na matatizo ya uzazi kutoka wastani wa Vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 (Mwaka 2015/2016) hadi kufikia wastani wa vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 (Mwaka 2022).
Pia Vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano vimepungua kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 (mwaka 2015/2016) hadi kufikia vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000 (Mwaka 2022).
Tunamshkuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa na uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya uliopelekea kupungua kwa kiwango kikubwa vifo vya mama wajawazito vinavyotokana na matatizo ya uzazi na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa kukabidhi vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Watoto Njiti) na watoto wachanga wagonjwa na wenye uzito pungufu. Vifaa na vifaa tiba hivyo vimefadhiliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation leo kwenye hospitali ya Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment