MKURUGENZI kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ndg. Jonas Masingija amesema kwamba miaka ishirini (20) ijayo Mkoa wa Shinyanga utakuwa ni kitovu cha usindikaji wa mazao ya mifugo, chakula na senta ya madini ukizingatia inakwenda kutumia vema mpango wa ardhi yake.
Masingija ameyasema haya leo tarehe 3 Septemba, 2024 alipokuwa akielezea moja kati ya mada katika mkutano wa Kuwasilisha na Kujadili Mpango wa Matumizi ya Ardhi wa Mkoa wa Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wataalam mbalimbali kutoka katika Halmazshauri 6 zinazounda Mkoa wa Shinyanga.
No comments:
Post a Comment