SAMIA ALAANI MAUAJI YA KIONGOZI WA CHADEMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 8 September 2024

SAMIA ALAANI MAUAJI YA KIONGOZI WA CHADEMA



Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani ameelezea masikitiko yake kufuatia kifo cha Kiongozi wa CHADEMA Mzee Mohamed Ali Kibao aliyekutwa ameuawa na kutupwa maeneo ya Ununio Kinondoni DAR es Salaam.


Rais Samia ameagiza uchunguzi wa haraka wa tukio hilo na mengine kama hayo.
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki"

"Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso