RAIS SAMIA -TUONGEZE UZALISHAJI WA KAHAWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 24 September 2024

RAIS SAMIA -TUONGEZE UZALISHAJI WA KAHAWA





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ametembea kichanja (dryer) cha kusafisha na kuanika Kahawa aina ya Arabica ya Kampuni ya AVIV Tanzania Limited tarehe 24 Septemba 2024 wakati wa ziara yake katika Shamba la kampuni hiyo.


Akiwa katika kichanja hicho Rais Samia amesema:


“Leo tunafurahia bei nzuri sana ya kahawa. Lakini soko hili haliko hivi hivi siku zote. Soko linapanda na kushuka. Kwa hiyo kwa ile miaka ambayo tunavuna vizuri kahawa, tunapata fedha nyingi, fedha zile tutumie na tuweke akiba. Kwa miaka ambayo soko litashuka, basi lisije likateteresha chumi zetu au hali yetu ya maisha. Niwaombe sana wakulima kote nchini na hii sio kahawa tu, hata mazao mengine tuende na mtindo huo".


“Huu ni mradi mkubwa unaoleta matumaini ndani ya nchi yetu. Lakini ukiacha uzalishaji mbunge amesema kwamba muwekezaji huyu amekuwa akitushika mkono kwenye mbalimbali ya afya, elimu maji na maeneo mengine katika vijiji vinavyomzunguuka. Sasa nami nataka nikubaliane na kauli ya Waziri kwamba kwenye maeneo yam aji, madaraja, madarasa, nyumba za madaktari, nyumba za walimu nadhani wamefanya za kutosha sasa twende kwenye kuongeza uzalishaji wa kilimo,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa katika kichanja (dryer) cha kusafisha na kuanika Kahawa aina ya Arabica ya Kampuni ya AVIV Tanzania Limited tarehe 24 Septemba 2024 wakati wa ziara yake katika Shamba la kampuni hiyo.


Zoezi hilo ni kwa ajili ya usindikaji wa Kahawa ili kupata muonjo bora ambao ndiyo unamuwezesha mkulima kupata bei nzuri sokoni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso