Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali itaendelea na ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege, barabara, na bandari ili kuvutia wawekezaji zaidi kuja kuwekeza nchini.
Dk. Mwinyi amefafanua kuwa Serikali inaendelea na mipango ya kuimarisha viwanja vya ndege, ikiwemo uwanja wa Pemba, ili kufungua milango zaidi kwa watalii na wawekezaji kuvutiwa kuja Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 21 Septemba 2024, alipofungua Hoteli ya Shukrani Palace iliyopo Michamvi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.
Aidha Rais Dk. Mwinyi ameipongeza menejimenti ya Taasisi ya Nada Group Hotels kwa kuwekeza nchini kupitia mradi huo mkubwa na ameahidi kwamba Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha unafanikiwa.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ametaja maeneo mengine ya kipaumbele kuwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri, Bandari ya Malindi, Mangapwani, na Shumba kisiwani Pemba, huku akisisitiza wananchi kuunga mkono juhudi hizo.
Vilevile Rais Mwinyi amewahimiza wawekezaji kuweka mkazo zaidi kwenye kununua bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa ndani ili kuwainua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment