RAIS MWINYI: TANZANIA NA MSUMBIJI ZITAENDELEA KUIMARISHA UDUGU WAKE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 7 September 2024

RAIS MWINYI: TANZANIA NA MSUMBIJI ZITAENDELEA KUIMARISHA UDUGU WAKE

 



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Tanzania ilitoa mchango mkubwa katika harakati za kupatikana kwa Uhuru wa Msumbiji, ikizingatiwa kwamba Chama cha Frelimo kilianzishwa Dar es Salaam mnamo mwaka 1962 chini ya uongozi wa Hayati Eduardo Chivambo Mondlane.


Aidha, Tanzania ilitoa mchango mkubwa kwa kuwafundisha wapiganaji wa chama hicho sambamba na kutoa askari wake kusaidia mapambano dhidi ya Wareno.


Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo katika Sherehe za Miaka 50 ya Siku ya Ushindi zilizofanyika katika kiwanja cha Matola, Msumbiji.


Vile vile, Rais Dk. Mwinyi amesema siku ya maadhimisho hayo yana umuhimu mkubwa kwetu sote kwa kutambua mchango wa Tanzania katika kusaidia kupata uhuru pamoja na kuwa sehemu ya historia hiyo.


Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Tanzania na Msumbiji zitaendelea kuimarisha uhusiano wake kwa sababu nchi hizo mbili zinashirikiana katika nyanja nyingi zikiwemo za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kitamaduni, na udugu uliopo.


Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi chake cha miaka 10 madarakani, hususan katika kujenga uchumi wa nchi hiyo. Pia, ameitakia Msumbiji uchaguzi mwema na wa amani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso