Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewaagiza Wakurugenzi na Wakuj wa Taasisi zote mkoani Shinyanga kuhakikisha kwamba Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano wanapelekwa kwenye mafunzo ya Lugha ya Alama ili waweze kusaidia mawasiliano katika utoaji wa huduma kwa wananchi wakiwemo makundi maalum kama viziwi.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 25 Septemba, 2024 alipokuwa akifungua Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani ambayo yalianza tarehe 23 Septemba, 2024 na Kitaifa yanafanyika hapa mkoani Shinyanga ufunguzi ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, Taasisi na watumishi ambao wamewezesha kuipamba shughuli hii huku akisisitiza kuwa lugha ya alama ni sawa na lugha nyingine duniani kama vile kichina nk.
"Nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi zote ndani ya Mkoa huu kuhakikisha wanawapeleka mafunzoni Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano ili waweze kusaidia mawasiliano na utoaji wa huduma kwa wananchi na hasa makundi maalum wakiwemo viziwi kwani hawa ni wenzetu na wanazo haki zote kama binadamu wengine," amesema RC Macha.
Akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni ili aseme neno, Mkuu wa Wilaya ya Kahama ambaye pia amekaimu Wilaya ya Shinyanga Mhe. Mboni Mhita amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa mtetezi mkubwa wa watu wote wakiwemo viziwi, jambo ambalo linawapa nguvu wao wasaidizi wake kuendelea kutafsiri vema maono ya Mhe. Rais kwa vitendo hukumakiwakaribisha wageni wote wilayani Shinyanga na kwamba usalama upo wa kutosha sana na wananchi wake ni wakarimu sana.
Kwa upande wake RAS CP. Hamduni amesema kuwa maadhimisho haya yalinza tarehe 23 Septemba, 2024 na yatahitimishwa rasmi tarehe 28 Septemba, 2024 ambapo yanatarajiwa kufungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (MB). Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Ungana Kutetea Haki za Lugha ya Alama".
Awali akitoa salamu za Chama cha Viziwi Tanzania Mwenyekiti Bi. Celina Mlemba amesema kuwa, maadhimisho haya ni utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa la tarehe 9 Disemba, 1917 la kuzitaka nchi wanachama kufanya maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani kila ifikapo Septemba ya kila mwaka.
No comments:
Post a Comment