MWANARIADHA ACHOMWA MOTO NA MPENZI WA ZAMANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 3 September 2024

MWANARIADHA ACHOMWA MOTO NA MPENZI WA ZAMANI




Mwanariadha chomwa moto na mpenzi wa zamani


Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei yuko katika hali mahututi katika hospitali moja nchini Kenya, baada ya kudaiwa kuchomwa na moto wa petroli na mpenzi wake wa zamani.
Mwanariadha


Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye alishiriki katika michezo ya Olimpiki ya hivi karibuni mjini Paris, ameungua kwa zaidi ya asilimia 75 ya mwili wake, polisi wamesema.


Alishambuliwa nyumbani kwake magharibi mwa Kenya, ambako alikuwa akifanya mazoezi.


Kuna wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa visa vya ukatili dhidi ya wanariadha wa nchini Kenya, baadhi yao vimesababisha vifo.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso