MONGELLA ATETA NA VIONGOZI WA MASHINA/ MATAWI KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 8 September 2024

MONGELLA ATETA NA VIONGOZI WA MASHINA/ MATAWI KAHAMA



Na Paul Kayanda,Kahama


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongela, amewataka viongozi wa chama hicho ngazi za mkoa na wilaya kushuka hadi ngazi za chini ili kuimarisha matawi, mashina, na mabalozii.


Akizungumza katika jengo la CCM la Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga,ambako alikwenda kwa lengo la kujitambulisha kwa wanachama wake, Mongela alisisitiza umuhimu wa viongozi hao ngazi za juu kufika kwa wananchi ambako ndiko chimbuko la nguvu ya chama.


Mongela alieleza kuwa ni lazima viongozi hao wawe karibu na wanachama wa ngazi za chini ili kuhakikisha uhai wa chama unadumu kwa kuzingatia maoni na matatizo ya wananchi.


"Ngazi za matawi na mashina ndizo msingi wa CCM, na viongozi wanapaswa kushuka mara kwa mara ili kuimarisha muunganiko kati ya chama na wananchi," alisema Mongela.


Ziara hiyo ya Mongela inakuja wakati ambapo chama kinaendelea na juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya viongozi na wanachama, hatua ambayo imepewa kipaumbele katika kuhakikisha ushindi wa CCM unaendelea kuwa imara katika chaguzi zijazo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso