NA PAUL KAYANDA, KAHAMA
Mkuu wa kituo ch Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, Mkaguzi Msaidizi Hafidhi Omari, ameendesha semina maalum katika Kituo cha Afya Kagongwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanawake kuhusu vyanzo vya moto majumbani, Lengo kuwasaidia wanawake kujikinga na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakisababisha hasara kubwa na kuhatarisha maisha katika jamii.
Omari alieleza vyanzo vya moto ni pamoja na uendeshaji wa shughuli za jikoni bila tahadhari kama matumizi ya gesi yasiyo salama, vifaa vya umeme visipofanyiwa matengenezo mara kwa mara vinavyoweza kusababisha moto ambapo ameshauri
kuwa na vifaa vya kuzima moto majumbani na kuelewa namna ya kutumia vifaa hivyo endapo kutatokea dharura.
Kina mama walioudhuria semina hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina juu ya hatua bora za kuchukua ili kujikinga na majanga ya moto. Aidha, walipongeza jitihada za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kutoa elimu hiyo muhimu ambayo itawasaidia katika kulinda maisha yao na mali zao.
Omari aliahidi kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu njia bora za kuzuia na kukabiliana na majanga ya moto ili kupunguza athari katika Wilaya ya Kahama.
No comments:
Post a Comment