MKALAMA YATANGAZA MKAKATI WA KUPAMBANA NA HOMA YA NYANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 5 September 2024

MKALAMA YATANGAZA MKAKATI WA KUPAMBANA NA HOMA YA NYANI





Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali amewataka Wakuu wa Idara, Watumishi wa Afya, Watendaji Kata na Vijiji pamoja na Maafisa Tarafa wilayani Mkalama kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujilinda na ugonjwa wa homa ya Nyani maarufu kama Mpox


Wito huo ameutoa Septemba 5,2024 wakati wa kikao cha afya ya Msingi wilayani Mkalama kilichofanyika kwenye ukumbi ulipo ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mkalama


"Wakuu wa Idara, watumishi wa afya, Watendaji kata na Vijiji pamoja na Maafisa Tarafa kwa pamoja twendeni tukaelimishe jamii kuhusu homa ya nyani na namna ya kujilinda na ugonjwa huu" DC Machali


Aidha katika kuhakikisha wananchi wanajilinda na ugonjwa huo, Mhe. Moses Machali amepiga marufuku wananchi kusalimiana kwa kupeana mikono ili kujilinda na ugonjwa huo "Kuanzia leo tusisalimiane kwa kupeana mikono, tukifanya hivi tutajilinda na sisi na kuwalinda wengine" Mhe. Machali


Vile vile Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ametoa agizo kuwekwa maji yanayotiririka pamoja na sabuni katika maeneo yote ya taasisi za umma pamoja na yale yenye watu wengi


Awali akiwasilisha hali ya ugonjwa huo, Afisa Afya Wilaya ya Mkalama Dorice Damiani amesema kuwa ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kushikana mikono, kujamiana na mtu mwenye ugonjwa huo pamoja na kuchangiana nguo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso