Mhe. Cosato Chumi aelekeza ushirikiano wa karibu na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 13 September 2024

Mhe. Cosato Chumi aelekeza ushirikiano wa karibu na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) amepokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Anne-Sophie Avé katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.


Mhe. Chumi amempongeza Mhe. Avé kwa kupewa jukumu hilo na kuahidi kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwake na Ubalozi wa Ufaransa ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi wawapo Tanzania.


Naye Balozi Mteule Avé amejidhatiti kukuza ushirikiano huu wa uwili hasa katika maeneo ya kimkakati ikiwemo nishati safi ya kupikia, utalii na ulinzi. Aidha amefurahishwa kuona Tanzania ikishika namba moja kwa sehemu inayotembelewa zaidi na watalii kutoka Ufaransa pamoja na fungate.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso