KIONGOZI WA CHADEMA ATEKWA KISHA KUUWAWA, POLISI YATHIBITISHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 8 September 2024

KIONGOZI WA CHADEMA ATEKWA KISHA KUUWAWA, POLISI YATHIBITISHA




Chanzo cha picha,CHADEMAMaelezo ya picha,Ally Mohamed Kibao alikua mjumbe wa Sekretariati ya Chadema taifa



Jeshi la polisi nchini Tanzania limethibitisha taarifa za kuuawa kwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Chadema, Ally Mohamed Kibao.


Taarifa za kutekwa zilitolewa na viongozi wa chama cha upinzani siku ya Jumamosi na baadae kusambaa katika mitandao ya kijamii.


‘’Jana Septemba 7,2024 Jeshi la Polisi lilitoa taarifa juu ya Ally Mohamed Kibao kushushwa kutoka kwenye basi la Tashrif na kuchukuliwa na watu ambao hawakuweza kutambulia na kwamba uchunguzi ulianza baada ya kupokelewa taarifa hiyo. Baada ya kutolewa taarifa za kuonekana mwili wa mtu mwanaume ambaye hakuweza kutambuliwa kwa wakati huo ni mwili wa nani huko Ununio Jijini Dar es Salaam, utambulizi umefanyika kwa mujibu wa taratibu na kubainika ni mwili wa Ally Mohamed Kibao.’’ Inaeleza taarifa ya jeshi hilo.


Kwa mujibu wa katibu wa chama hicho John Mnyika alisema kuwa Mzee Ali kibao alikua safirini aliekea mkoani Tanga kabla ya kuchukuliwa na watu wenye silaha na pingu kisha kumshusha kwa nguvu.


‘’Jana majira ya saa 12 jioni lilitokea tukio ninaliita la kutekwa siyo kukamatwa kwa Mzee Ali Mohamed Kibao ambaye ni mjumbe wa Sekretariati ya Chadema taifa, tukio hilo limetokea maeneo ya Kibo karibu na Tegeta, Mzee Kibao akiwa anasafiri kutoka Dar es salaam kwenda Tanga, basi hilo lilizuiwa na gari mbili, walishuka watu wakiwa na silaha na kumwambia dereva asiondoe basi, kisha kwenda kwenye kiti alichokaa na kumchukua kwa nguvu" Alisema Mnyika’’.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso