DOTTO MAGARI AWATAKA CHADEMA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KUDUMISHA AMANI NCHINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 16 September 2024

DOTTO MAGARI AWATAKA CHADEMA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KUDUMISHA AMANI NCHINI

 






Na Mwandishi wetu

Mfanyabiashara maarufu wa magari nchini Tanzania, Dotto Keto maarufu kama 'Dotto Magari', amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kudumisha amani nchini.


Amesisitiza umuhimu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha siasa za upotoshaji na badala yake kumshukuru Rais Samia kwa kazi kubwa anayofanya kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Magari amesema "Nyinyi majirani zetu mlikuwa hamna ofisi kwa takribani miaka 30, leo Mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa Mikocheni mnataka nini majirani?"

Aidha Magari amewataka CHADEMA kumuunga mkono Rais Samia kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.

“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia, hiyo siyo amani? . Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi”

“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba mama Samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi” ,amesisitiza

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso