Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ametembelea na kukagua ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania, Kampasi ya Mwanza, inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha, kwa gharama ya shilingi bilioni 7.8, kitakachokuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi zaidi ya 5,000 kwa wakati mmoja, na kuahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwekeza rasilimali fedha katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.
Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Pallangyo, alieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali kupitia Wizara ya Fedha, imekipatia Chuo hicho shilingi bilioni 58.1 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia katika Kampasi zake nane za Mtwara (bil. 6.1). Mbeya (Bil 3.2), Mwanza (bilioni 7.8), Kigoma (bilioni 11) na Zanzibar (sh. bilioni 30).
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) yuko katika ziara ya kikazi ya siku 7 mkoani Mwanza, ambapo atafanya shughui za kukagua, kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment