CHAVIZA YAADHIMISHA KILELE CHA WIKI YA VIZIWI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 30 September 2024

CHAVIZA YAADHIMISHA KILELE CHA WIKI YA VIZIWI






WANACHAMA wa Chama cha Viziwi CHAVIZA wakipita kwa maandamano kuelekea katika kilele maadhimisho ya wiki ya viziwi Duniani, ambayo kwa upande wa Zanzibar yalifanyika Jongowe Wilaya ndogo Tumbatu.


KATIBU mtendaji Baraza la taifa la watu wenye ulemavu, Mhandisi Ussi Khamis Debe, akizungumza katika kilele cha wiki ya viziwi Duniani, hafla iliyofanyika Jongowe Wilaya ndogo Tumbatu kwa upande wa Zanzibar. 

(PICHA NA FAUZIA MUSSA).


NA FAUZIA MUSSA


WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais, Harusi Said Suleiman, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dk. Husein Ali Mwinyi itaendelea kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu ili kushiriki katika harakati mbali mbali za maendeleo nchini.


Akizungumza kwa niaba ya Waziri huyo, katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi Duniani yaliyofanyika Jongowe Wilaya ndogo Tumbatu, Katibu mtendaji Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar, Mhandisi Ussi Khamis Debe alisema hatua hiyo itasaidia katika kuhakikisha ushiriki na ushirikishwaji wa watu hao kwenye nyanja mbalimbali za kimaendeleo unaonekana.


Alisema ili kufanikisha adhma hiyo ni lazima jamii ijifunze lugha ya alama ili kurahisisha mawasiliano kwa kundi hilo hali itakayosaidia kurahisisha ushiriki na ushikishwaji wao katika harakati za maendeleo ya taifa.


alisema endapo jamii Itakua na uelewa WA lugha ya alama tasaidia katua changamoto mbalimbali zinazowakabili kundi Hilo.


“watu viziwi wanahaki ya kikatiba kama watu wengine katika nyanza zote za kimaendeleo nchini ni vyema wakathaminiwa na kupewa kipaumbele katika familia na ngazi zote.”Alisema mhandisi Debe


Wakati huo huo alikitaka chama cha viziwi kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kupata fursa ya mikopo inayotolewa kwaajili yao (four four two) na kujikwamua kiuchumi.


“asilimia 2 za fedha zinazo kusanywa na manispaa ni kwaajili yenu andaeni vikundi na mufuate taratibu za kupata fedha hizo kwa misingi ya kujikwamua kimaisha.”


Mwenyekiti wa chama cha viziwi CHAVIZA Asha Ali Haji , na Katibu wa chama hicho Abdalla Alawi Abdalla, walisema viziwi bado wanakabiliwa na changamoto ya mawasiliano ndani ya jamii kutokana na kutokujua lugha ya alama kuweza kuwasiliana nao.


Walisema kundi hilo linakosa walimu wa kutosha Maskulini, vyuo vikuu na hata madrasa hali inayowafanya kutoshiriki ipasavyo katika kutafuta elimu na kuziomba Serikali kulipa umuhimu suala la lugha ya alama kwa jamii ili kupata haki zao kama wanavyopata wengine


Walieleza kuwa kukosekana kwa wakalimani katika baadhi ya sehemu za kutolea huduma za jamii kama hospital, sehemu za biashara katika vyombo vya usafiri kunawakosesha kupata taarifa muhimu ipasavyo zinazotolewa katika maeneo hayo.


Mbali na hayo waliiomba Serikali na wadau wa maendeleo kuwasaidia kupata jengo la ofisi la chama hicho ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo.


Katibu Tawala Wilaya ndogo Tumbatu, Khatib Habibu Ali, aliwapongeza wanachama cha chaviza kwa kufanya hafla hiyo kijijini Tumbatu jambo ambalo alilitaja kuleta mwamko wa jamii ya kijiji hicho kuona umuhimu wa kundi hilo na kuleta mabadiliko.


Aidha katibu huyo aliasa jamii kutowaficha watoto wenye ulemavu kwani wanapaswa kupata haki za msingi kama wanavyopata watoto wengine.


Mapema katibu tawala alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Husein Ali Mwinyi, kwa jitihada za maendeleo zinazoendelea nchini pamoja nakuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu katika nyanza zote za maendeleo hayo.


Wiki ya viziwi Duniani huadhimishwa kila ifikapo wiki ya mwisho ya Septemba, kwa lengo la kuiunganisha jamii ya viziwi na kuwa na sauti moja ya kutetea haki zao wote, ambapo kauli mbiu yam waka huu ni “UNGANA KUTETEA HAKI ZA LUGHA YA ALAMA”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso