Kampeni ya chanjo dhidi ya Mpox nchini DRC inatarajiwa kuaanza Oktoba 2, huku wafanyakazi wakilenga majimbo matatu yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huo.
Mratibu wa Kamati ya Majibu ya Monkeypox ya Congo, Cris Kacita Osako, amesema watu wazima katika majimbo ya Equateur, Kivu Kusini na Sankuru watapewa chanjo ya kwanza mwezi ujao.
Mapema wiki hii, kundi la kwanza la chanjo ya mpox liliwasili katika mji mkuu wa Congo, kitovu cha mlipuko huo.
No comments:
Post a Comment