AWESO AMTUMBUA MENEJA WA RUWASA MISUNGWI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 9 September 2024

AWESO AMTUMBUA MENEJA WA RUWASA MISUNGWI




Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amemuondoa katika nafasi yake Meneja wa RUWASA wilayani Misungwi Mhandisi Marwa Kisibo kutokana na kutosimamia utekelezaji wa miradi ipasavyo katika wilaya yake.

Waziri Aweso amefanya maamuzi hayo alipotembelea Mradi wa Maji wa Ukiliguru - Usagara - Kolomije - Sumve wa Chanzo cha Ziwa Victoria unaogharimu kiasi cha zaidi ya Bilioni 32 wilayani Misungwi na Kwimba Mkoa wa Mwanza.

Ziara hii ni Maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi alipofanya ziara yake mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi na kupata malalamiko ya hali ya upatikanaji Maji na kusuasua kwa Miradi. Dkt Nchimbi alimuelekeza Aweso kufika Misungwi na kufanyia kazi changamoto zote.

Aidha Aweso amezungumza na viongozi na wananchi wa Wilaya ya Misungwi na kutoa maelekezo mahususi ikiwa ni pamoja na Kuhakikisha mkandarasi wa mradi anafanya kazi usiku na mchana ili kazi hii ikamilike kwa wakati na kumuagiza Katibu Mkuu na Mtendaji mkuu wa RUWASA Wakae na mkandarasi anayejenga mradi huo Emirates Builders siku ya  tarehe 09/09/2024 pamoja na Wakandarasi wote wanaotekeleza Miradi ya Maji wilaya ya Misungwi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso