Na. Paul Kasembo, USHETU.
IKIWA ni siku ya nne ya tangu kuanza kwa zoezi la Uboreahaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Jimbo la Ushetu muitikio ni mzuri sana na hakuna shida iliyojitokeza mpaka leo ambapo Mratibu wa Uboreshaji Mkoa wa Shinyanga ndg. Bakari Kasinyo amefika na kutembelea zaidi ya Vijiji 16 ili kuona namna ambavyo zoezi linavyotekelezwa.
Kwa nyakati tofauti na sehemu tofauti tofauti alizofika ndg. Kasinyo pamoja na maelekezo, ushauri na mapendekezo mengine lakini ameonesha kuridhishwa na utekelezaji wa zoezi hili huku akitoa wito wa kila mmoja kwa nafasi yake kuendelea kutoa hamasa na elimu kwa wananchi kuzitumia vema siku hizi zilizobakia.
Zoezi la Uboreahaji wa Daftari la Mpiga kura kwa Mkoa wa Shinyanga ulianza rasmi tarehe 21 Agosti, 2024 na utakamilika ifikapo tarehe 27 Agosti, 2024 huku wito ukitolewa na viongozi na wadau mbalimbali kwa wananchi kujitokeza kupata huduma hii ambayo inaanza kila siku saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni kwa vituo vyote.
No comments:
Post a Comment