TUME YA HURU YA UCHAGUZI IMEKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI MKOA WA SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 9 August 2024

TUME YA HURU YA UCHAGUZI IMEKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI MKOA WA SHINYANGA

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura

NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL BLOG 

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ukiongozwa na kauli mbiu 'Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora'.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliofanyika leo Ijumaa Agosti 9,2024 Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk  Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, amesema mkutano huo umelenga kupeana taarifa mbalimbali za maandalizi kwa ajili ya kuanza rasmi kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari.

“Lengo hasa la kukutana na wadau ni kupeana taarifa za uwepo wa zoezi hili na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni,  tutapeana taarifa juu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, na maandalizi hayo pamoja na mambo mengine yanajumuisha uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura, uboreshaji wa majaribio, ununuzi wa vifaa na ushirikishwaji,”amesema Jaji Mbarouk.

Washiriki wa mkutano katika mkoa wa Shinyanga ni   Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.

"Tume imepewa jukumu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika jamhuri ya Muungano pamoja na Madiwani kwa upande wa Tanzania Bara", amesema Jaji Mbarouk .

Jaji Mbarouk ameeleza kuwa wataandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu 2025, pia kutakuwa na fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye daftari na ambao wamehama wanaweza kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Seleman Mtibora ambaye amewasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoani Shinyanga, amesema kwa kuzingatia Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, wapiga kura 5,586,433 wapya wanatarajiwa kuandikishwa sawa na asilimia 18.7 ya wapiga kura 29,754,699 waliopo kwenye daftari baada ya uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/20 na kwamba wapiga kura 4,369,531 inatarajiwa wataboresha taarifa zao.

"Wapiga kura wapya wanaotarajiwa kuandikishwa katika Mkoa wa Shinyanga ni 209,951 na waliopo katika daftari la kudumu la wapiga kura ni 995,918, hivyo tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Shinyanga utakuwa na wapiga kura 1,205,869",amesema Mtibora.

"Mkoa wa Shinyanga kuna vituo 1,339 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 122 katika vituo1,217 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/2020", ameongeza Mtibora

Aidha, mzunguko wa pili wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaendelea sasa katika mikoa ya Kagera na Geita ambapo uboreshaji ulianza tarehe 5 hadi 11 Agosti, 2024.

Tume tayari imeanza zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo uzinduzi ulifanyika mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 na mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB). Uzinduzi huo ulienda sambamba na kuanza kwa mzunguko wa kwanza wa uboreshaji kwenye mikoa mitatu ya Kigoma, Tabora na Katavi.

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo Ijumaa Agosti 9,2024 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga 

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso