Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imewaasa wadau wa biashara kuzingatia elimu ya mabadiliko ya sheria mpya ya ukusanyaji wa mapato ili waweze kutekeleza majukumu yao ya ulipaji kodi kwa hiyari.
Mafunzo hayo yametolewa agosti 22, 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya kahama ambapo ilijumuisha waandishi wa habari, wadau na wafanyabiashara lengo kuwajulisha wafanya biashara kuhusu mabadiliko ya kodi kwa mwaka 2024/2025.
Afisa wa TRA Wilaya ya kahama amesema kupewa taxclearence hakumaanishi kwamba mfanyabiashara hadaiwi, anaweza kupewa kwa makubaliamo ya kulipa tararibu.
"kwa mwaka huu wa kodi 2024/2025 serikali inatarajia kukusanya tilioni 49.35 ya mapato ambapo TRA pekee inatakiwa kukusanya tilion 39", amesema afisa wa TRA.
Cpa Lucy Ashery ameomba semina na elimu kutoka TRA kuboreshwa, kodi ni sehemu kubwa ya pato la nchi kwa hiyo wafanya biashara wengi wamekuwa hawana elimu kuhusu kulipa kodi.
Mmoja wa wafanyabiashara waliopata elimu ya mabadilikoa ya kodi Jeremia Samson ameipongeza TRA kwa kutoa elimu pia ameiomba TRA kuhimiza zaidi wafanya biashara kutumia mashine za kutolea risiti kwani wafanya biashara wengi wanaamini kuwa kwa kutumia mashine kunawasababishia hasara.
Aidha jeremia amewataka wafanyabiashara wenzake kujitokeza pale wanapoambiwa kuna semina au mafunzo kuhusu TRA kwani itawasaidia kulinda biashara zao.
No comments:
Post a Comment