Baadhi ya washabiki wa timu ya yanga, walimu na wanafunzi wa shule ya Ilindi wakipiga picha ya pamoja baada ya kupewa zawadi kama madaftari ,sabuni,kalami nk. Kama inavyoonekana katika picha
NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA
Tawi la Yanga mtaa wa Ilindi, Manispaa ya Kahama, limefanya usafi katika mazingira ya shule na kutoa msaada wa vifaa vya shule ikiwemo madaftari, kalamu za wino, penseli vichongeo, taulo za kike pamoja na sabuni kwa baadhi wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilindi.
Mkuu wa shule ya Ilindi Mwalimu Abeid Meza amewapongeza wanachama wa Yanga tawi la Ilindi kwa kujitoa, wameonesha moyo wa ukarimu pia amewakaribisha na wengine kuleta msaada katika shule hiyo kwani kuna wanafunzi baadhi wanamahitaji maalum.
Alisema shule yake imeweza kufika katika hatua ya mashindano ya kitaifa katika michezo (UMITASHUMITA), na wanafunzi watatu wamechaguliwa na TFF kwa ajili ya mafunzo zaidi huko Tanga.
Makamu Mwenyekiti wa tawi la Yanga Samike Guma alieleza kuwa msaada huo uliogharimu zaidi ya shilingi laki nne, msaada huo umeletwa kama sehemu ya kujipongeza kwa ushindi wa timu yao na kupata makombe mengi.
Mwanafunzi wa shule hiyo Inocent Geofrey amewapongeza wanachama wa Yanga kwa msaada waliouleta, akisema kuwa msaada huo unawahamasisha katika masomo na michezo.
Pia mwanafunzi mwingine Annastazia Obed amesema wanayanga wamewatia moyo katika masomo na michezo kwani michezo ni ajira hivyo wataendelea kuonyesha vipaji vyao zaidi.
Sambamba na hilo Mkuu wa shule hiyo amesema shule yake ina zaidi ya watoto elfu tatu(3735) ambapo inakabiliwa na upungufi wa vyumba vya madarasa na vyoo
Mmoja kati ya wanafunzi waliochaguliwa na TFF kuendelea na mafunzo ya kimchezo huko Tanga baada ya kuwa washindi katika mashindano ya umitashumita kwa ngazi ya Taifa
Mmoja kati ya wanafunzi waliochaguliwa na TFF kuendelea na mafunzo ya kimchezo huko Tanga baada ya kuwa washindi katika mashindano ya umitashumita kwa ngazi ya Taifa
Mashabiki wa yanga wakifanya usafi wa mazingira pamoja na kuchoma takataka katika shule ya msingi Ilindi iliyopo Manispaa ya Kahama
No comments:
Post a Comment