TANZANIA YAONGEZA NGUVU KINYANG'ANYIRO NAFASI YA UKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA:UJUMBE MAALUM WAWASILI CONGO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 25 August 2024

TANZANIA YAONGEZA NGUVU KINYANG'ANYIRO NAFASI YA UKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA:UJUMBE MAALUM WAWASILI CONGO

 



Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo, wamewasili Jijini Brazzaville, Congo wakiwa pamoja na ujumbe maalum wa Tanzania kwa ajili ya kumnadi mgombea wa Tanzania, Dkt. Faustine Ndugulile (Mb.), anayewania nafasi ya Ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika. Hii ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 74 wa WHO Kanda ya Afrika unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.




Katika mkutano huu muhimu, ujumbe wa Tanzania unajumuisha wataalamu na viongozi kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wajumbe hawa wanatarajia kushiriki mikutano ya pembezoni ili kujadili masuala muhimu na kuhakikisha upatikanaji wa kura kutoka kwa nchi wanachama wapatao 47 wa WHO.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso