TAKUKURU:MGOMBEA MTOA RUSHWA HAWEZI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI,SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 7 August 2024

TAKUKURU:MGOMBEA MTOA RUSHWA HAWEZI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI,SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI




TAKUKURU:MGOMBEA MTOA RUSHWA HAWEZI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI, SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI


Na Marco Maduhu,SHINYANGA
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga, imewatahadharisha wananchi wawe makini katika chaguzi zijazo, kwa kuchagua wagombea wenye sifa na uwezo wa kuwaletea maendeleo na siyo watoa rushwa.


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy amebainisha hayo leo Agosti 7,2024 katika ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari mkoani humo, inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya rushwa.
Amesema kuwa ni muhimu kwa waandishi wa habari kutoa elimu kwa wananchi, ili waweze kufanya maamuzi sahihi katika chaguzi zijazo, ukiwami wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani 2025.


Kessy alisisitiza kwamba rushwa inatishia demokrasia na inawanyima wananchi haki yao ya kupata viongozi waadilifu.
"Wagombea watoa rushwa hawawezi kuwaletea maendeleo wananchi, na vitendo vya rushwa vinaweza kuondoa nafasi za wagombea wenye sifa," amesema Kessy.


“Wananchi wanapaswa kuwa na ufahamu wa kutosha ili waweze kufanya maamuzi sahihi na kuchagua viongozi wanaofaa,”ameongeza Kessy.
Pia,amewataka waandishi wa habari kuzingatia maadili katika kazi zao na kuepuka kutumiwa na baadhi ya wanasiasa, ambao wanajaribu kuwapatia rushwa ili kuandika habari zinazompamba mgombea asiyefaa au kumchafua mwingine.


Endelea kufuatilia mtandao huu kwa habari zaidi hapo baadae………..

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso