RAIS SAMIA TUUNGE MKONO UJENZI WA OFISI YETU YA KISASA - MASHABIKI WA YANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 19 August 2024

RAIS SAMIA TUUNGE MKONO UJENZI WA OFISI YETU YA KISASA - MASHABIKI WA YANGA



Mwenyekiti wa umoja wa kikundi cha mashabiki wa timu ya Yanga katika kijiji cha Bumbiti, Kata ya Mondo, Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga, Masunga Ndimali, amemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kusaidia katika ujenzi wa ofisi yao ya kisasa, ambayo inatarajiwa kujengwa hivi karibuni.


Mwenyekiti huyo alitoa ombi hilo mbele ya mgeni rasmi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Kamati Tendaji ya Wilaya ya Kahama, Emmanuel Alphonce, wakati wa sherehe za kikundi hicho ambazo zililenga kuanzisha tawi la Yanga na kutambuliwa na viongozi wa wilaya.


Aidha, mwenyekiti huyo alieleza kuwa tawi hilo lina zaidi ya wanachama 85 ambao wanatakiwa kupewa kadi za uanachama wa chama hicho. Pamoja na mambo mengine, mwenyekiti huyo alieleza kuwa mdau mmoja wa michezo kijijini hapo, mkazi wa Sangilwa aitwaye Joseph Kusoka, amejitolea kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ya kisasa kwa shughuli za michezo kijijini hapo, na kazi iliyobaki ni kuanza ujenzi mara moja. Mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Samia awaunge mkono katika kufanikisha ujenzi huo.


Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, licha ya kumuomba Rais Samia msaada huo, pia aliomba migodi midogo midogo iliyoko kijijini hapo kuguswa kwa namna moja ama nyingine ili kufanikisha upatikanaji wa ofisi hiyo ya kisasa.


Hata hivyo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Kamati Tendaji ya Wilaya, Emmanuel Alphonce, aliwataka wanachama wa tawi hilo jipya kuendelea kujiunga kwa wingi, akiwakumbusha kuwa ili kuwa mwanachama kamili, lazima uwe na kadi za chama, ambazo zinapatikana kwa gharama ya shilingi 34,000 kupitia Benki ya NBC.


Kiongozi huyo alibainisha kuwa, kwa Wilaya ya Kahama nzima, kuna wanachama halali zaidi ya 500. Katika hafla hiyo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Kamati Tendaji ya Wilaya ya Kahama aliendesha harambee ya dharura na kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi 500,000, pamoja na vifaa vya ujenzi kama mifuko ya saruji, nondo, mabati, na mchanga.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso