RAIS SAMIA AAGIZA HUDUMA ZOTE ZA KIJAMII ZIREJESHWE NGORONGORO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 23 August 2024

RAIS SAMIA AAGIZA HUDUMA ZOTE ZA KIJAMII ZIREJESHWE NGORONGORO



OR-TAMISEMI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza kurejeshwa kwa huduma za kijamii ikiwamo za elimu na afya zilizokuwa zimezorota katika Tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi ameyasema hayo leo Agosti 23, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata 11 zilizopo Tarafa ya Ngorongoro kuhusu maagizo ya Mhe. Rais Samia aliyewatuma kuwasikiliza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku tano wakitaka kujua hatma ya malalamiko yao.


Mhe. Lukuvi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngorongoro kuhakikisha vyoo vya Shule vilivyokuwa vimetitia na kupelekea wanafunzi kujisaidia vichakani vijengwe upya na mashine ya kusuma

Maji katika shule ya Wasichana ya Ngorongoro iliyokuwa imeharibika na kusababisha wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata maji itengenezwe.



Pia, amesema Rais Samia anataka huduma za afya na elimu zirejee kikamilifu na kuelekeza halmashauri fedha zilizopo zitumike kurekebisha kasoro zote zilizokuwapo ili wananchi wapate huduma bora katika vijiji na vitongoji vya Tarafa ya Ngorongoro.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso