RAIS MWINYI AZINDUA KIJANA NA KIJANI ZANZIBAR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 10 August 2024

RAIS MWINYI AZINDUA KIJANA NA KIJANI ZANZIBAR







Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amewahakishia Vijana kuwa Serikali imekusudia fungu la fedha ili kuwawezesha katika Elimu , Ajira na Uwezeshaji.




Rais Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 10 Agost 2024 katika Uwanja wa New Complex Amaan wakati wa alipozindua kampeni ya kijana kijani ya Tunazima zote Tunawasha kijani iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi .




Aidha Rais Dk.Mwinyi ameleeza kuwa katika kuwainua Vijana Serikali iweka mkazo katika maeneo matatu ambayo Ongezeko la Ajira, fungu la Mikopo kuwafikia vijana na nafasi za uteuzi za Uongozi.







Dk.Mwinyi amewahimiza vijana kujipanga na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za Uongozi katika Vyombo vya Maamuzi na Serikali itawaunga mkono.







Ametumia fursa hiyo kuvishauri Vyama Upinzani kujifunza kwa Uvccm namna Bora ya kufanya Siasa na kuupongeza Umoja wa vijana kwa kazi nzuri.




Kwa upande mwingine Dk.Mwinyi amewapokea Wanachama 368 kutoka Vyama vya ACT Wazalendo na CUF waliojiunga na CCM wakiongozwa na Ndugu Ahmed Omar aliyewahi kuwa Msaidizi wa Maalim Seif Shariff Hamad na Juma Duni Haji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso