Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) Wilayani Kahama yameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwa kuzingatia maadili, mila na desturi za Mtanzania.
Hayo yamesemwa na Bakari Juma Kibile Mwenyekiti wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilaya Kahama Agosti 21, 2024, katika risala ya mashirika hayo kwenye Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) lililofanyika katika Ukumbi wa Mganga Mkuu-Hospitali ya Wilaya kahama
Bakari Amesema Sekta ya Mashirika Yasiyo ya KiserikaliWilayani Kahama imeendelea kukua na kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo mpaka sasa kuna mashirika zaidi ya 40 katika Wilaya ya Kahama ambayo yalisajiliwa kwa Afua
tofauti tofauti za mazingira, afya, kusaidia waraibu wa madawa ya kulevya, uwezeshaji mabinti kiuchumi, ujasiliamali, elimu, kilimo, utawala bora na haki za binadamu.
Bakari ameongeza kuwa pamoja na mchango huo mkubwa unaotolewa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Jamii, Sekta hii inakabiliwa na changamoto zifuatazo;-Upungufu wa rasilimali, Hii ni kwa rasilimali zote yaani watu na fedha, ukosefu wa wataalamu wa kutosha katika kuandika miradi hali inayopelekea mashirika mengi kusua sua.
Ukosefu wa vyanzo vya ndani vya mapato, Mashirika mengi yamekuwa yakitegemea rasilimali fedha kutoka kwa mfadhili hivyo pale fedha ya mfadhili inapokosekana basi na shirika husika husimamisha shughuli zake za kuisaidia Jamii piaUkosefu wa Wafadhili wa Fedha (Donors)
Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Wilaya ya Kahama yanaendelea kushirikiana na kushauriana na Wasajili wasaidizi toka Halmashauri zote za Kahama Manispaa, Ushetu DC na Msalala DC ili kuhakikisha tunapunguza changamoto
zilizondani ya uwezo wetu kwa mfano kuanzisha mwamvuli wa pamoja (Kahama NonGovernmental Organization Network).
Kwa upande wake, Mwakilishi NACONGO Wilaya ya Kahama Catherine Kalinga amemuomba mkuu wa wilaya ya Kahama kuwa na vikao viwili au vitatu kwa mwaka ili kuweza kutambuana na kueleza changamoto zinazowakabili kwa ni kuna mashirika mengine ni machanga.
Mgeni rasmi katika jukwa hilo Mkuu wa Wilaya ya Kahama mheshimiwa Mboni Mhita, ameyapongeza mashirika hayo kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuahidi ushirikiano kati ya serikali na NGOs ambapo ataandaa kikao cha kikanuni ili kusikiliza changamoto, maoni, uboreshaji yaani vile wanavyotamani kusaidiwa na ofisi yake.
"Natamani kuona mashirika yasiyo ya kiserikali katika wilaya wa kahama yanakua pia mashirika yasiyo ya kiserikali yanakwenda moja kwa moja katika jamii kwa hiyo lazima nifatilie kujua mtu anayekwenda katika jamii ni mtu sahihi?,
kwani tuko kwenye vita ya maadili na changamoto ya kukosoa mila na desturi, mimi nadhani kama kuna kitu cha kutuunganisha sio makabila sio dini bali ni utanzania wetu", amesema DC Mboni.
Kauli mbiu ya jukwaa hilo inasema "MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI NI WADAU MUHIMU, WASHIRIKISHWE KUIMARISHA UTAWALA BORA
No comments:
Post a Comment