MPOX SIO COVID 19 MPYA UNAWEZA KUZUILIKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 20 August 2024

MPOX SIO COVID 19 MPYA UNAWEZA KUZUILIKA




Ugonjwa mpya wa mpox uligundulika hivi karibuni nchini DRC Congo ambao teyari umeshauwa watu takribani 450 nchini. WHO wanesema mpox haiwezi kuwa kama COVID 19, sababu Mamlaka zinajua namna ya kuuzuia.


Tangu mlipuko wa ugonjwa huo uanze umeleta taharuki na mijadala maeneo mbalimbali ya Dunia, wataalamu wa afya nchi za Magharibi wanaamini ya kwamba licha ya uhatari wa ugonjwa huo MPOX ila hawataraji kuwa utakuwa janga la Dunia kama COVID 19.


Wataalamu wanaendelea kusema Mpox hautakuwa janga la Dunia endapo nchi na mamlaka za afya Duniani zikishirikiana pamoja kupambana kuuzuia mambukizi mapya na kuwatibu waathirika.


Msemaji wa WHO Tarik Jasarevic amesema mpox una chanjo teyari na chanjo itatolewa kwa waathirika na wale walio kwenye maeneo ya hatari kufikiwa na ugonjwa huo na sio watu wote.


Pia ameongezea kusema hakuna ulazima wa matumizi ya barakoa na hapatakuwa na karantini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso