MHE. DKT. NCHEMBA: SERIKALI KUTOA FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI WILAYANI MBULU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 23 August 2024

MHE. DKT. NCHEMBA: SERIKALI KUTOA FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI WILAYANI MBULU


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alikuwa Mgeni Rasmi katika Jubilee ya kutimiza miaka 25 ya Upadre ya Mhashamu Askofu Antony Gasper Lagwen, wa Jimbo Katoliki Mbulu iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, Mjini Mbulu Mkoani Manyara, ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara yenye urefu wa kilometa 50 itakayojengwa kwa kiwango lami kutoka Hydom – Labay hadi Garbabi kuanzia robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha (2024/2025). 


Barabara hiyo inatajiwa kugharimu shilingi bilioni 12 na itakapokamilika itarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wakazi wa wilaya hiyo na mkoa wa Manyara kwa ujumla.


Mhashamu Askofu Antony Gasper Lagwen, alizaliwa wilayani Mbulu Mkoani Manyara Mwaka 1967 na alipata Upadre mnamo mwaka 1999 na baadae kuwa Askofu mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso