Mbunge wa Ushetu Emanuel Cherehani akizungumza katika baraza la madiwani wa halmashauri ya Ushetu agosti 28, 2024, akilitaka jeshi la polisi kushirikiana na sungusungu ili kupambana na wizi wa mifugo.
NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL BLOG USHETU
Mbunge wa Ushetu Emanuel Cherehani amelitaka jeshi la polisi Ushetu kufanya kazi na sungusungu kama timu ili kukomesha wizi wa mifugo unaoendelea katika jimbo hilo.
Akizungumza leo agosti 28, 2024 katika baraza la madiwani wa Halmashauri ya Ushetu, amesema wananchi wanaibiwa mifugo hadharani huku akilitaka jeshi la polisi kutumia nafasi zao kwa kushilikiana na sungusungu kutatua changamoto hii.
"Napata taarifa nyingi hasa Bulungwa, wananchi wanaibiwa mifugo hadharan, wananchi na sungusungu wanafanya kazi kwa nguvu sana wanakamata watuhumiwa lakini wanakimbilia polisi ambapo sungusungu wanakamatwa wao na watuhumiwa kuachiwa", amesema Cherehani.
Naye Esther Matone, diwani viti maalumu kata ya Bulungwa amesema vijana wakienda kuchunga wanaibiwa ng'ombe kisga kuzichinja na kupeleka buchani au kusafirisha hali inayopelekea wafugaji kupata hasara.
Pia Tabu Katoto, diwani wa kata ya Igunda amesema polisi kwa kushirikiana na sungusungu wataweza kuwakamata wake wanaofunga nyama kwenye maboksi na kusafirisha bila taarifa kuwa nyama hiyo inechinjiwa wapi na imepimwa na nani, hiyo inaashiria kuwa ni wizi wa mifugo.
No comments:
Post a Comment