MAVUNDE AYATAKA MABENKI KUIUNGA MKONO BENKI YA CRDB KUWAKOPESHA WACHIMBAJI MADINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 19 August 2024

MAVUNDE AYATAKA MABENKI KUIUNGA MKONO BENKI YA CRDB KUWAKOPESHA WACHIMBAJI MADINI

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga

NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL KAHAMA

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ameipongeza Benki ya CRDB kwa kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wakiwamo wadogo na kuyataka mabenki na taasisinyingine za fedha kuiga mfano huo.

Mheshimiwa Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo leo mjini Kahama alikokabidhiwa ripoti ya utoaji huduma za fedha kwa wachimbaji wadogo na wa kati kutokana na maelekezo aliyoyatoa mwaka jana alipokutana na watendaji wa benki za biashara nchini.

“Wachimbaji wadogo ni jeshi kubwa kwenye sekta ya madini nchini lakini lenye changamoto ya mtaji. Iwapo benki zetu za ndani zitawapa kipaumbele watu hawa kama mnavyofanya Benki ya CRDB, mchango wa sekta ya madini kwenye pato letu la taifa utaongezeka kwa kiasi kikubwa. Nawapongeza Benki ya CRDB kwa kuuona umuhimu wa kuizingatia sekta hii,” amesema Mheshimiwa Waziri Mavunde.

Mwaka jana, Mheshimiwa Waziri Mavunde aliwaeleza watendaji wa mabenki nchini juu ya changamoto ya upatikanaji wa huduma za fedha ikiwamo mikopo kwa wachimbaji wadogo na kuwataka kuangalia namna ya kurahisisha upatikanaji wake ili kukuza mchango wa sekta ya madini nchini ambayo inaajiri maelfu ya wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.

Kwenye hafla hii, Mheshimiwa Waziri Mavunde amesema Serikali itandelea kuimarisha mazingira yauchimbaji nchini ikiwamo kujenga uwezo wa wachimbaji wadogo kufanya utafiti utakaowasaidia kuchimba maeneo yenye uhakika wa kupaa madini tofauti na hali ilivyo sasa wanapochimba kwa kubahatisha.

Serikali inaendelea na juhudi za kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kutekeleza mikakati tofauti kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuwa inatambua kuwa bado wachimbaji wadogo wengi wanafanya shughuli zao bila kufanya utafiti wa kisayansi hivyo kutokuwa na uhakika wa kupata madini wanayoyakusudia,” amesema Mheshimiwa Waziri Mavunde.

Waziri Mavunde amesema hayo baada ya Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa kumjulisha kuhusu hatua kadhaa zilizofanywa na benki katika kuwawezesha wachimbaji wadogo pamoja na changamoto ilizokutana nazo.

Akiainisha mchango wa Benki ya CRDB, Raballa amesema imeanzisha kitengo maalum cha madini ili kutoa wigo mpana wa utekelezaji wa mikakati inayoelekezwa kwenye sekta ya madini na kujenga uwezo kwa wafanyakazi kuchambua maombi na mahitaji ya wachimbaji wadogo wa madini.

Kitengo hiki, Raballa amesema kinasaidia kuratibu utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa wachimbaji wadogo ambayo wanaipata kwa wakati unaostahili, benki inawapa huduma za bima, inafadhili ununuzi na uingizaji wa kemikali pamoja na mitambo muhimu ya uchakataji na uchenjuaji madini nchini na inawasaidia kubadili fedha za kigeni kila inapohitajika.

“Benki yetu imeendelea kuwa mstari wa mbele kufanikisha upatikanaji wa fedha za uwekezaji wa miradi ya madini kuanzia kwa wachimbaji wadogo mpaka wakubwa. Hadi sasa tumeshakopesha zaidi ya shilingi bilioni 64. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 19 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo,” amesema Raballa.

Kwa wachimbaji wakubwa, afisa huyo amesema Benki ya CRDB imeidhinisha mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 120 kwenye mradi wa uchimbaji wa madini ya kinywe unaotekelezwa na kampuni ya Faru Graphite na imeteuliwa kuongoza jopo la mabenki kutafuta fedha za ujenzi wa mradi uchimbaji wa madini ya urani utakaogharimu dola milioni 900 za Marekani baada ya kuthibitishwa na Tume ya Madini.

“Benki yetu pia imeanzisha kitengo maalumu kinachosimamia mnyororo wa thamani ambacho moja ya majukumu yake ni kuwaunganisha watu na fursa zilizopo kwa kuhakikisha kinaboresha mahusiano na huduma zetu kuwafikia hadi wateja kwa wakati sahihi. Hata hivyo, kati ya changamoto kubwa zilizopo ni wachimbaji wadogo kutotunza kumbukumbu za uzalishaji na mauzo ya madini jambo linaloweza kuwaongezea vigezo vya kupata mikopo kwa urahisi,” amesema Raballa.

Naye Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha amesema mkoa wa Shinyanga ni moja ya mikoa ya kimadini ambao unatambua mchango wa sekta ya madini ambapo katika mwaka wa 2023/2024 ulifikisha asilimia 85 ya ukusanyaji wa maduhuli hivyo upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo utachochea shughuli za uchimbaji wa madini ambao utasaidia kuongezeka kwa mapato ya serikali.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Masache Kasaka ameipongeza Wizara ya Madini na taasisi zake kwa juhudi mbalimbali inazofanya katika mageuzi makubwa ndani ya sekta ya madini ikiwa ni sehemu ya maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Kamati ikiwemo hilo la kusimamia upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo.

Akitoa salamu, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania (FEMATA)  ,John Wambura Bina amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Madini ambao umeanza kuleta tija na kuaminika kwa wachimbaji wadogo kukopesheka kwakuwa sasa kuna mashine za uchorongaji zinazosaidia kupata taarifa za awali za uwepo wa madini na hivyo kuwatoa wachumbaji kwenye kuchimba kwa kubahatisha.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa Mheshimiwa Waziri Mavunde kukabidhi mfano wa hundi kwa baadhi ya wachimbaji wa kanda ya ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka.

Kuhusu Benki ya CRDB

Benki ya CRDB ni moja benki zinazoongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki, inatoa huduma kwa wateja wadogo, wakati na wakubwa ikiwamo huduma kwa wateja binafsi, huduma za hazina, huduma za bima, mikopo ya biashara, kilimo na uwezeshaji kwa wajasiriamali wadogo.

Benki ya CRDB ndio benki ya kwanza nchini Tanzania kutambuliwa na kampuni ya kimataifa ya utafiti ya Moody’s Investors Service kuwa moja kati ya benki 10 imara na salama Afrika katika uwekezaji. Moody’s imeipa Benki ya CRDB daraja la uimara la B1 ambapo ni daraja la juu zaidi kupatikana kwa mabenki na taasisi za fedha katika ukanda wa jangwa la Sahara. Benki ya CRDB imepata utambuzi wa Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UN Green Climate Fund) tangu mwaka 2019 na pia imetambuliwa kama benki bora Tanzania na jarida la Global Finance kwa mwaka 2020 na mwaka 2022 ilitambuliwa kama benki bora Tanzania na jarida la Euromoney.

Benki ya CRDB imekuwa kiungo muhimu cha biashara katika nchi za Tanzania, Burundi na DRC kwa kuwahudumia wateja zaidi ya milioni 4 na kupitia mtandao mpana wa matawi zaidi ya 260, zaidi ya CRDB Wakala 25,000, 550 ATM, mashine za manunuzi 1,800 na Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachotoa huduma saa 24/7.

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akielezea hatua kadhaa zilizofanywa na benki katika kuwawezesha wachimbaji wadogo pamoja na changamoto ilizokutana nazo.

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony (mwenye tai nyekundu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini nchini (FEMATA), John Bina akizungumzawakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akitoa salamu wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akitoa salamu wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini Mhe. Masanche Kasaka akizungumzawakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe. Hussein Kassu akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Kamishna wa Madini nchini, Dkt. Abdulrahman Mwanga akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga
Wadau wa Sekta ya Madini wakiwa kwenye kikao

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (mwenye suti ya bluu) akiangalia kikundi cha burudani ya ngoma ya utamaduni ya Kabila la Wasukuma
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (mwenye suti ya bluu) akiangalia kikundi cha burudani ya ngoma ya utamaduni ya Kabila la Wasukuma
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (mwenye suti ya bluu) akitoa zawadi kwa kikundi cha burudani ya ngoma ya utamaduni ya Kabila la Wasukuma
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (kushoto),Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (kushoto), akisaimiana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso